KARIBU
MASHATI RURAL
SACCOS LIMITED
KARIBU
Mashati Rural
Saccos Limited
Mashati Rural Savings and Credit Cooperative Society Limited (Mashati Rural SACCOS Ltd) ni Chama cha Ushirika wa wa Akiba na mikopo kinachoundwa na fungamano la Wakulima, Wafanyabiashara, Wafugaji na Wafanyakazi; kilichoanzishwa na kusajiliwa tarehe 18 Septemba 1998 na kupewa nambari ya usajili KLR 496 na sasa ina nambari PRI-KJR-ROM-DC-2022-1433 na Leseni Daraja” B” Nambari MSP3-TCDC-2002-0031
Lengo kuu la Mashati Rural SACCOS Ltd ni kuwezesha ustawi wa kiuchumi na kijamii kwa Wanachama
Huduma Zetu
Mashati Rural Saccos Inatoa Huduma Za Mikopo Kwa Wanachama Wake Ya Aina Mbalimbali Pia Kiasi Na Muda Wa Marejesho Hutegemeana Na Aina Ya Mkopo Mkopaji Anaoomba Katika Mashati Rural Saccos Ltd
Hiki ni kiasi cha fedha ambacho mwanachama anajiwekea katika akaunti yake mara kwa mara kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya baadaye kwa kadri ya uwezo wake. Mwanachama anaweza kujiwekea michango hii kutoka kwenye mishahara au fedha taslimu.
Hisa huwakilisha sehemu ya umiliki wa chama.
Mwanahisa ana haki ya kupata gawio kutoka kwenye faida kwa kiwango kilichoamriwa kigawiwe na mkutano mkuu.
Mwanahisa ana haki ya kupiga kura kwenye mkutano mkuu wa chama kulingana na taratibu za chama.
Ni akaunti ya mawekezo ya mwanachama ambapo Mwanachama anafungua kwa ajili ya malengo tofauti tofauti na anaweza Kutoa pesa kila mara anapohitaji.
Mwanachama anaweza kuweka kila mwezi au mara kwa mara kulingana na malengo atakayokuwa nayo.
Mashati Rural SACCOS – Kikokotoo cha Mkopo
Kokotoa Mkopo Wako
Kokotoa Mkopo Wako
Wanachama
Bidhaa za Mikopo
Mali
Mtaji
Ushuhuda wa Wateja
Nilipata mkopo wa biashara kutoka Mashati Rural SACCOS na uliinua biashara yangu kwa kiwango kikubwa. Masharti ni rafiki, riba iko wazi kwa njia ya salio, na huduma ni ya haraka. Ni taasisi ya kuaminika kwa maendeleo ya mwanachama.
Mashati Rural SACCOS imenisaidia sana katika kilimo changu kupitia mkopo wa kilimo na ufugaji. Niliweza kununua pembejeo kwa wakati na kuongeza uzalishaji. Ushirikiano na ushauri wao ni wa kiwango cha juu
Ninapenda uwazi na uongozi wa Mashati Rural SACCOS. Viongozi wanawajali wanachama na maamuzi hufanywa kwa demokrasia. Kamati na bodi zinafanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa
Nilipopata changamoto ya dharura, Mashati Rural SACCOS ilinisaidia kwa mkopo wa dharura kwa haraka sana. Mchakato ni rahisi na marejesho ni yenye kueleweka. Hii ni taasisi inayojali ustawi wa wanachama wake.
Unahitaji Msaada wa Haraka?
Piga simu +255 756 399 958
Wafanyakazi wetu wako tayari kukupa msaada wa haraka na kukusaidia wakati wowote unapohitaji kwa siku 7 kwa wiki.